Image
Image

Kesi ya mita 200 kwa mpiga kura kusikilizwa tena leo mahakama kuu.

Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam imeahirisha kesi ya kikatiba kuhusu kutoa tafsiri ya umbali wanaotakiwa kusimama wapiga kura baada ya kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu ili kutoa muda kwa upande wa serikali kuandaa majibu.
Awali katika Kesi hiyo inayoongozwa na jaji Sakieti Kihiyo, Aloysious Mujulizi na Lugano Mwandambo walimtaka wakili wa mpigakura Amy Kibatala, aliyefungua kesi hiyo kubadilisha hati ya mashitaka kutoka kwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na kuielekeza kwa mkurugenzi wa tume ya uchaguzi ambaye ndiye mwangalizi wa masuala yote ya uchaguzi.
Kwa upande wao wadaiwa katika kesi hiyo upande wa serikali ikiongozwa na wakili Obadia Kameya umeiomba mahakama kuipa muda mpaka saa nane mchana hii jana ili waweze kuwasilisha majibu ya maombi ya kesi hiyo.
Katika kesi hiyo namba 37 ya mwaka 2015 inayosimamiwa na wakili Peter Kibatala inaiomba mahakama kutoa tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha sheria ya taifa ya uchaguzi kuhusu umbali ambao mpiga kura anastahili kukaa kutoka kituo cha kupigia kura.
Jaji Sakieti Kihiyo ambaye ni mwenyekiti wa kesi hiyo ameahirisha kesi hiyo mpaka leo saa tatu itakaposikilizwa tena.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment