Image
Image

Nape Nnauye amepata ajali mbaya Lindi.


KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi 
(CCM), Nape Nnauye amepata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea 
Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.

Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi  alipata 
ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya 
Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la 
Nyangao mkoani Lindi.

Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha 
gari hilo ambapo amepata majeraha madogo  ila anaendelea vizuri.

Akizungumza na mtandao huu, Nape amesema: "Namshukuru Mungu nimetoka 
salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya 
maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na 
michubuko ila ni mzima.


Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na 'air bag' nazo zimenisaidia."

Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo 
aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli 
aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya 
shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo 
lake la Mtama.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment