Image
Image

NEC:Waliopoteza kadi zao za kupigia kura hawataruhusiwa kupiga kura.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema wapiga kura waliopoteza kadi zao za kupigia kura hawataruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika nchini kote siku ya Jumapili.
Akizungumza katika mkutano wa vyama vya siasa na NEC mjini Dodoma leo, Ofisa Mwandamizi wa tume hiyo William Kitebi, amesema watu hao hawataruhusiwa hata kama majina na taarifa zao zipo kwenye Daftari la Wapiga Kura (BVR).
"Hakuna jinsi ya kuwasaidia watu waliopoteza kadi zao za kupigia kura ,"amesema Kitebi
Hata hivyo, Kitebi amesema kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye BVR  kuna baadhi ya mambo NEC wameyawekea utaratibu ili watu waweze kupiga kura.
Amesema watu ambao namba za kadi zinatofautiana na zile zilizopo kwenye BVR  lakini taarifa nyingine ni sahihi wataruhusiwa kupiga kura.
"Kuna wale ambao picha zao hazionekani kwenye daftari lakini kadi za kupiga kura wanazo, hawa wataruhusiwa kupiga kura,"amesema.
Kuhusu wale wapiga kura walioathiriwa na mipaka ya utawala, Kitebi amesema maamuzi ya tume kuwa watu hao watapiga kura kwenye kata walizopo.
"Kuna maeneo kulikuwa na mabadiliko ya mipaka ya kiutawala baada ya zoezi la uandikishaji kama Kishapu (Shinyanga) na Kaliuwa (Tabora), wao wataruhusiwa kupiga kura kwenye maeneo yao mapya,"amesema.
Kwa upande wa wapiga kura ambao wanakadi za kupigia kura lakini hawaonekani kwenye BVR, Kitebi amesema hao wamewekewa utaratibu utakaowawezesha kupiga kura.
"Kama kule Mbarali (Mkoa wa Mbeya), kuna watu kama 6,000 ambao hawaonekani katika daftari lakini wanakadi na fomu zao zimejazwa na kuwasilishwa tume  hawa wanaruhusiwa kupiga kura,"amesema.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment