Image
Image

Polisi yawaondoa hofu wananchi wakati wa upigaji kura Morogoro.

Polisi Mkoani Morogoro limewaondoa hofu wananchi  na kuwataka watumie haki yao ya msingi kujitokeza kupiga kura na kuwaonya wasijihusishe ña mikusanyiko y o  yote baada ya kupiga kura katika maeneo ya vituo vya kupiga kura.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro , LEONARD PAULO amesema hayo wakati kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ilipotembelea kituo kikuu cha polisi kuangalia maandalizi yanayofanywa na jeshi hilo kuelekea uchaguzi mkuu  kesho-kutwa.
Kamanda PAULO  amesema jeshi hilo limejipanga kwa vifaa vya kutosha kuhakikisha hakuna uvunjifu wo   wote wa amani utakaojitokeza na kwamba wanaamini uchaguzi huo utafanyika kwa amani  na utulivu .
Nao wananchi wa Mkoa wa Morogoro pamoja na kuahidi kujitokeza kupiga kura,   wameeleza imani yao kwa jeshi la polisi katika kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo .

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment