Image
Image

Serikali Mkoani Shinyanga imejipanga kuhakikisha mchakato mzima wa uchaguzi unakuwa huru na haki.

                   Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ALLY NASORO RUFUNGA.
Serikali Mkoani Shinyanga imejipanga kuhakikisha mchakato mzima wa uchaguzi unakuwa huru na haki.
Aidha Jeshi la Polisi mkoani humo limesema kuwa limejipanga kukakikisha amani  inatawala katika kipindi chote cha mchakato wa kupiga kura hadi matokeo kutangazwa na atakayefanya vitendo vya kuvuruga amani atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Wakizungumza baada ya kikao cha kujadili hali ya amani katika siku ya kupiga kura kilichowashirikisha wadau wa amani, viongozi wa vyama vya siasa na wakuu wa idara mbalimbali  za serikali baadhi ya washiriki wa vyama vya siasa wamepinga maelekezo yaliyotolewa na  Tume ya Taifa ya Uchaguzi na baadhi yaviongozi wa serikali siku chache zilizopita kuhusu wananchi kupiga kura na kuondoka vituoni.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ALLY NASORO RUFUNGA amesema ni vyema maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yakafuatwa ili kuufanya uchaguzi kuwa huru na amani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment