Image
Image

Viongozi wa vyama vya siasa waitupia lawama tume ya Taifa ya Uchaguzi,Kagera.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa Mkoani Kagera wameitupia lawama Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushindwa kusambaza mapema  elimu juu ya mambo yaliyopaswa kuzingatiwa  na wananchi na viongozi wa vyama vya siasa katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia hatua ya uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi hadi wakati wa zoezi  la upigaji kura.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakati wa semina maalumu iliyoandaliwa tume kwa viongozi wa vyama vya siasa mkoani humo, iliyokuwa na lengo la  kujadili matatizo mbalimbali yanayohusiana  na mwenendo mzima wa uchaguzi  wamesema,  ukosefu wa elimu ya kutosha miongoni mwa wananchi  juu ya masuala yanayohusu uchaguzi kuwa  ndio sababu  inayoigharimu tume ya hiyo  katika kutoa maelekezo ambayo wakati mwingine yamekuwa yakipingwa.
Katibu wa chama  cha NCCR-Mageuzi wa Mkoa wa Kagera,  PETERSON MSHEMELA  ameeleza  kuwa chama chake kitalinda kura kwa nguvu zote na kitaendelea kuwahamasisha wananchi wabaki kwenye vituo baada ya kupiga kura.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuia ya Umoja wa Vijana ya Chama cha Mapinduzi, Wilaya ya Bukoba  Mjini, GEORGE SANKA amewahimiza wapigakura waondoke nyumbani baada ya kupiga kura wakasubuiri matokeo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment