Image
Image

Watanzania zaidi ya Elfu-Moja na 660 wenye asili ya Rwanda na Burundi kutopiga kura.

Watanzania zaidi ya Elfu-Moja na 660  wenye asili ya nchi za Rwanda na Burundi wenye uraia wa kuandikishwa wanaoishi  Mkoani Kagera huenda wasishiriki kwenye zoezi la upigaji kura.
Hiyo inatokana na zoezi linaloendelea hivi sasa linalofanywa na Idara ya Uhamiaji hapa nchini la kuhakiki uhalali vibali vyao vya kuishi nchini lililoanza tangu mwaka 2006 iwapo  litadumu hadi siku ya upigaji wa kura.
Akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na Idara ya Uhamiaji Mkoani Kagera kwa maofisa wa idara hiyo,  juu ya elimu ya uraia na haki ya mpiga kura,  Naibu Kamishiina wa Uhamiaji,  JUSTINE  KEWISA amesema idara hiyo ilifikia uamuzi wa  kuhakiki  vibali hivyo,  baada ya kubaini udanganyifu uliokuwa ukifanywa na baadhi ya raia hao wa kughushi vibali hivyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera,  JOHN MONGELLA  amewataka maofisa uhamiaji  katika  kipindi hiki cha uchaguzi wasimamie sheria na wasikubali kuyumbishwa na wanasiasa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment