Image
Image

Breaking News:Mahakama yamwachilia huru Sheikh Ponda Issa Ponda Morogoro.


Hatimaye Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro imemuachilia huru kiongozi wa taasisi na jumuiya za kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda.aliyekuwa akikabiliwa Mashitaka matatu aliyokuwa anadaiwa kuyatenda Agost 2013 ambapo alikuwa akishitakiwa kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya dini nyingine na kushawishi watu kutenda kosa.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Mery Moyo amemuachia Sheikh Ponda huru baada ya kutoridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Mashtaka ikilinganishwa na hati ambayo iliyokuwa imemfungulia mashtaka awali.
Awali hakimu moyo alisema kwamba Sheikh Ponda alikuwa na mashtaka matatu shitaka la kwanza lilikuwa ni kutotii amri ya awali ya Mahakama na hivyo kuendelea kutoa mihadhara,Kushawishi watu kutenda kosa na shitaka la mwisho kuumiza imani ya dini zingine lakini ushaidi uliotolewa mahakamani hapo kwa mujibu wa hakimu moyo ulikuwa unazungumzia zaidi maneno ya uchochezi tofauti na maelekezo ya haki ya mashtaka ambayo yenyewe ilipelekwa mahakamani hapo kuwa Sheikh.Ponda alikuwa akifanya mkusanyiko usio halali.
Upande wa mashitaka haukuweza kubadili chochote wakati shitaka lilipokuwa likiendelea hii ikiwa ni kwa mujibu wa Sheria,hivyo makosa aliyokuwa nayo kuonekana hayagusi ile hati mashitaka iliyokuwa ikizungumzia kufanya mkusanyiko usio halali.
Sheikh Ponda alikuwa akitetewa na mawakili Juma Nasoro,Abubakar Salim na Bartholomeo Tarimo,ambapo katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa ukiwakilishwa na wakili wa serikali mwandamizi Benard Kongola, Sunday Hyera na george Mbalasa.
Endelea kufuatilia taarifa zetu kila zinapotufikia,Like Page yetu kupata habari zaidi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment