Image
Image

Breaking News:Waziri mkuu aagiza waliohusika na upotevu wa makontena 349 bandari ya DSM kukamatwa.


Waziri mkuu wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam na kuona hali ilivyo katika utendaji kazi na hivyo kuagiza waliohusika na upotevu wa makontena 349 kukamatwa mara moja.

Katika ziara hiyo ya kushtukiza waziri mkuu huyo alitaka kujua namna ya kupokea mizigo hapo bandarini na namna ambavyo mamlaka ya mapato Tanzania na mamlaka ya bandari (TPA) namna wanavyoshirikiana kuhakikisha kwamba kodi stahiki inalipwa kulingana na mizigo inawasili bandarini hapo.

Vile vile alitaka kujua kwamba kwanini kunakuwepo na mwanya wa upotevu wa mapato na pia kwanini baadhi ya wafanya biashara inadfaiwa kuwa wanatoa mizigo bandarini bila ya kuli[pia ushuru ama bila kulipa kodi inayo stahili na kwa wakati,na pia kutaka kujua ninani anayesababisha hali hiyo ya watu kutoa mizigo bandarini bila kulipia kodi inayotakiwa.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa ambaye amekuwa na kiu ya kutaka kujua mambo kadhaa bandarini hapo amesema na kwa kuhoji Mamlaka ya Bandari naTRA kuwa wanahakikisha vipi kwamba mizigo inayo daiwa kwenda nje ya nchi inakuwa ni mizigo inayo pita njia halali bila ujanja ujanja uaotumika kutokana na kuwa na madai kuwa baadhi ya mizigo imekuwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi huwa haifiki inaishia hapa hapa mjini na mwishowe kuuzwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment