Image
Image

Kaya zaidi ya 40,000 Arusha zahitaji msaada.


Kaya ya 40.000 zilizoko  katika  vijiji  361  vya  mkoa wa Arusha zinakabiliwa na umaskini  mkubwa wa kipato unaochangiwa  na  kushuka kwa  uzalishaji  wa  kilimo  na  mifugo na asilima  kubwa  ya  wananchi  hawana uwezo wa kughaharimia matibabu na elimu kwa  watoto wao.

Wananchi  wa baadhi ya vijiji  vinavyokabiliwa na tatizo hilo  wamesema pamoja  na serikali  kuwapatia ruzuku bado ni kubwa  kutokana  na uweza  mdogo wa kubuni  miradi  inayoweza kuwa  endelevu.

Aidha wananchi  hao wameiomba serikali kutumia wataalam wake  kuangalia upya namna  ya kupata ufumbuzi wa kudumu ukiwemo  wa  kuziba mianya  inayochangia  kuongezeka kwa umaskini badala  ya kuendelea  kupunguza  makali.

Wakizungumzia changamoto  hiyo  walipokuwa wanazindua awamu ya  tatu ya  mpango wa kuzisaidia kaya maskini  katika wilaya ya monduli  baadhi  ya  viongozi  na  watendaji  wa serikali wa  mkoa wa Arusha wamesema zaidi  ya  shilingi  bilioni  1.7 zimetengwa kupunguza  makali ya  tatizo hilo ambapo  wilaya ya Monduli  yenye  kaya  zaidi   ya  milioni  6,242  imetengewa milioni .

Mkuu  wa  mkoa  wa Arusha Bw.Felexs Ntebenda amezitaka idara  zinazohusika  kuendelea  kuwatambua wananchi wanaokabiliwa na hali  mbaya  ili serikali  iweze  kuchukua  hatua  na  amesema hakutakuwa  na huruma  na yeyote atakayedhubutu kutumia  fedha zinazotolewa   kinyume  na  utaratibu   na  amewaomba  wananchi  kutoa  ushirikiano.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment