Image
Image
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis anatarajiwa kuanza ziara yake barani Afrika siku ya Jumatano juma hili
Nchi atakayozuru mwanza itakuwa ni Kenya kati ya tarehe 25 hadi 27. Mamilioni ya watu wanatarajiwa kushiriki misa itakayoongozwa na Papa Francis jijini Nairobi.


Baada ya Kenya, Papa Francis atazuru Uganda na kumalizia ziara yake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Novemba 25
Ndege itakayombeba kiongozi huyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa Kimataifa wa ndege wa JKIA Jumatano Novemba 25 mwendo wa saa kumi na moja jioni.
Baada ya kutua atalakiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na viongozi wengine wa serikali na kidini. Ataelekea katika Ikulu ya Rais kwa mazungumzo na mwenyeji wake, viongozi wa kisiasa na wanadiplomasia hapo saa kumi na mbili jioni na kisha baadaye wawil hao watalihutubia taifa la Kenya.
Novemba 26
Siku ya pili Alhamisi tarehe 26 Baba Mtakatifu atakutana na viongozi wa dini mbali mbali hapo saa mbili asubuhi kisha ataongoza misa ya hadhara katika chuo kikuu cha Nairobi kuanzia saa nne na baadaye kuwa na mkutano wa kiekumeni na makasisi wa Katoliki kuanzia saa kumi kasorobo. Itimiapo saa kumi na moja na nusu jioni Papa Francis atazuru makao makuu ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira, UNEP katika eneo la Gigiri mjini Nairobi ambako natarajiwa kutoa tamko kubwa kuhusu mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Novemba 27
Mnamo Ijumaa tarehe 27 ambayo itakuwa siku ya tatu ya ziara yake nchini Kenya Papa Francis atazuru mtaa wa Kangemi ambao una makazi duni na ambapo atakutana na wanakijiji elfu moja mia mbili baada ya hapo ataelekea Uwanja wa Kasarani ambako atakuwa na mkutano na vijana wa Kenya. Baadaye saa tano na robo atakutana na maaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya katika uwanja huo huo wa Kasarani.
Mwendo wa saa tisa na dakika kumi atafanyiwa sherehe ya kumuaga katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKIA na kuondoka baadaye kuelekea nchini Uganda.
Atalakiwa katika uwanja wa Entebbe na kuelekea katika Ikulu ya Rais wa Uganda ambako atafanya mazungumzo na mabalozi , baadaye atalihutubia taifa la Uganda. Saa moja na robo jioni atafika katika uwanja wa Munyonyo ambako atakutana na waalimu na kutoa hotuba.
Novemba 28
Jumamosi tarehe 28 akiwa baado nchini Uganda atazuru madhabahu ya waanglikana katika eneo la Namugongo hapo saa mbili asubuhi na kisha kuzuru madhabahu ya wakatoliki katika eneo lilo hilo. Ataangoza misa ya hadhara kwa kumbukumbu ya Mashuhuda wa Uganda mwendo wa saa tatu na nusu nna kukutana na vijana wa Uganda katika Uwanja wa ndege wa Kololo na baadaye kutembelea makao ya kutoa misaada kwa watoto huko Nalukolongo , baadaye atakutana na maaskofu wa kanisa Katoliki katika afisi ya Askofu Mkuu na kukutana muda mfupi baadaye na makasisi wakatoliki mwendo wa saa moja jioni.
Novemba 29
Hapo Jumapili tarehe 29 Papa Francis atakamilisha ziara yake nchini Uganda saa tatu asubuhi na kuelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako atawasili katika uwanja wa kimataifa wa "M'Poko" mjini Bangui atapokelewa na Rais na kuelekea ikulu ya Rais atakutana na mabalozi na viongozi wengine na kutoa hotuba na kisha baadaye kuzuru kambi ya wakamibizi.
Baadaye atakutana na maaskofu wa kanisa katoliki na kukutana na viongozi wa dini mbali mbali katika chuo kikuu cha Bangui. Ataongoza misa ya hadhara katika Kanisa kuu la Bangui na kutoa hotuba.
Mida za saa moja jioni ataongoza shughuli ya kuungama kwa dhambi miongoni mwa vijana na badaye aongoze hafla ya maombi ya kukesha katika kanisa kuu la Bangui. Ataondoka baadaye kuelekea Rome, Italia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment