Image
Image

Waziri Mkuu Majaliwa Ataka Majibu ya kina kwanini magari ya mwendo kasi hayaanzi kazi.


Waziri mkuu Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa ameshangazwa na kitendo cha mradi wa mabasi yaendayo kasi kutokuanza kazi hadi hivi sasa licha yakuelezwa kuwa katika ripoti kuwa kila kitu kimekamilika.

Akiongea kwa msisitizo wenye muonekano wa Ukali Waziri Majaliwa amewataka Katibu mkuu,Mkurugenzi na Afisa wake kufika Ofisini kwake kesho saa nne ili kueleza kwanini mradi huo bado na nilini mradi huo utaanza kazi rasmi.

“Nataka kujua nilini mradi huu utaanza kazi kwanini mpaka leo mabasi hayajaanza kazi,nani ana kwamisha huu ni mradi wetu wa TAMISEMI”Amesema Majaliwa.

Amesema majibu hayo yatatoa maelezo yakina hata kama jambo hilo litagusa taasisi hiyo ya TAMISEMI na kama kuna watu wamezuia watajua ni kwanini kwani mradi huu ukikwama watanzania wanajua ni TAMISEMI hivyo hawajui kama ndani yake kuna kitengo kimoja baada ya kingine kinachozuia mchakato huo kuanza mara moja.

Mradi huo unatakiwa kuanza kwani wamewekeza fedha nyingi na hivyo amesema kuwa sasaivi taa za barabarani zipo vizuri zinaongoza magari lakini magari hayo ya mwendo kasi hayaanzi kazi hadi ya haribike jambo ambalo anasema sio sawa anahitaji majibu ya kina.

Mshangao huo umekuja muda mfupi baada ya kutembelea katika ofisi za TAMISEMI na kukutana  na wakurugenzi wake na kusema kuwa watanzania wanasubiri mradi huo kwa ham kubwa lakini hakieleweki kitu kinacho kwamisha mradi huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment