Saratani ya shingo ya kizazi ni tatizo hatari linaloweza kusababisha
kifo ambalo husababishwa na virusi viitwavyo 'Human Papilloma Virus'
(HPV)
Zifuatazo ni sababu ambazo huweza kumuweka mwanamke katika hatari ya kukubwa na saratani ya shingo ya kizazi.
Kujihusisha na ngono wakati wa umri mdogo
Wasichana
wanaoanza kujamiana wakiwa na umri mdogo wako katika hatari ya kupata
saratani hii ya shingo ya kizazi. Hivyo ni vyema kuepuka kujihusisha na
ngono ukiwa na umri mdogo.
Kuwa na mahusiano na wapenzi wengi
Mwanamke
mwenye wapenzi wengi au mwenye mwanaume ambaye anawapenzi wengi yote
hayo huchangia kumuweka mwanamke katika hatari kubwa ya kupata saratani
ya shingo ya kizazi .
Kujifungu watoto wengi.
Wale kinamama
ambao hujifungua watoto wengi, huweza kuwa katika hatari ya kukubwa na
tatizo hili la saratani ya shingo ya kizazi, ndio maana baadhi ya
wataalam wamekuwa wakishauri angalau mama anapofikisha watoto watano
akasitisha zoezi la kuendelea kuzaa.
Historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia.
Aina hii ya saratani pia huhusishwa sana na masuala ya kurithishwa katika familia ya mgonjwa husika.
Upungufu wa kinga za mwilini
Magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga mwilini kama Ukimwi huweza kuchangia mhusika kupata saratani hii kwa urahisi zaidi .
Mbali
na sababu hizo dalili au viashiria vya saratani ya shingo ya kizazi ni
pamoja na kutokwa damu katika tupu ya mwanamke (uke) ambayo si ya
kawaida inaweza kuwa matone au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa
hedhi (yaani baada ya hedhi au kabla ya hedhi inayofuata).
Dalili nyingine ni kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa, lakini pia unaweza kupata maumivu makali wakati wa kujamiana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment