Image
Image

Latest News:Abiria wakwama kituo cha mabasi ubungo kwa kukosa usafiri.




Abiria wanaosafiri kuelekea katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania wamekwama katika kituo cha mabasi ya abiria ubungo jijini Dar es Salaam kutokana na magari kuwa machache haswa kwa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwaajili ya kwenda kusalimu ndugu jamaa na marafiki.
Tambarare Halisi imeshuhudia ugumu wa upatikanaji wa mabasi hayo yanayo enda mikoa mbali mbali nchini jambo ambalo limesababisha abiria kugombea gari moja ili kuweza kupata nafasi na kusafiri waendako.
Licha ya ugumumu wa mabasi abiria wameonekana kuwa wengi mnoo haswa ikizingatiwa kuwa ni siku chache tu zimebaki ili kusherehekea sikukuu ya Xmass na Mwaka mpya,ambapo abiria hao wengi wakionekana kuwa na watoto wadogo hali ambayo imeonekana kuogofya usalama wa watoto hao kituoni hapo.
Nauli kwa kiasi flani zimetajwa kuwa juu maradufu kwa baadhi ya abiria kulipa kiasi kikubwa cha fedha ilikuwahi,lakini jeshi la polisi limeonekana kuwepo eneo hilo,huku mamlaka ya usafiri nchi kavu na majini Sumatra wakiendelea kutoa vibali hadi daladala bila mafanikio ya kupunguza tatizo hilo.Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mohamed Mpinga amesema lengo la jeshi hilo kufika kituoni hapo nikuhakikisha kuwa abiria waliopo eneo hilo wanasafiri kwa usalama wa hali ya juu licha ya uchache wa magari yaliyopo.
Pia Kamanda Mpinga amewaasa abiria kutokusita kutoa taarifa dhidi ya Dereva anayeendesha gari kwa mwendo wa kasi na kuhatarisha usalama wao,kwa kupiga ama kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba 0800757575 ili dereva huyo achukuliwe hatua mara moja.
Amesema kipindi hiki cha mwisho wa mwaka madereva wamekuwa wakiendesha magari kwa mwendo wakasi na ikizingatiwa kipindi hiki huwa ajali nyingi hutokea na kupoteza maisha ya watanzania bila sababu kutokana na uzembe wa dereva anayejaribu kuendesha gari kwa mwendo wa kasi ili kuwahi kufika.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment