Image
Image

Mali: hali ya tahadhari hadi Januari 1.


Mali imewekwa rasmi tangu Jumanne hii katika hali ya tahadhari hadi mwanzoni mwa mwezi Januari mwakani, ikiwa ni kwa mara ya pili tangu shambulio dhidi ya hoteli moja ya kifahari mjini Bamako mwezi Novemba, wakati ambapo wanajihadi kadhaa "wameangamizwa" na jeshi la Ufaransa.
Aidha, katika ripoti, kitengo cha Haki za Binadamu cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa UN nchini Mali (Minusma) kimelaani "ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa" katika mashambulizi ya kijiji kimoja, kaskazini mwa nchi. Mashambulizi ambayo yanadaiwa kutekelezwa na makundi ya Azawad (CMA, kundi la waasi lenye watu wengi kutoka jamii ya Watuareg), na wakati kijiji hicho kilipowekwa chini ya himaya ya vikosi vya serikali.
Raia wawili waliuawa wakati wa shambulio lililoendeshwa na waasi wa CMA katika kijiji cha Tin Hama, na siku iliyofuata, raia wengine sita waliuawa, na jamii, ambayo inatuhumiwa kuunga mkono waasi, ilifukuzwa kwa vitisho. Karibu watu 230, kulingana na ripoti hiyo, ilithibitisha taarifa zilizokusanywa wakati huo baina ya wahusika wakuu.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) unalaani ukiukaji wa sheria za kimataifa na makundi ya waasi na kusikitishwa hasa kuona hakuna uchunguzi wa mahakama ulioanzishwa, na vile vile upande wa vikosi vya kijeshi, na kudai uchunguzi wa serikali "kuhusu tabia ya askari walio kuwepo katika kijiji cha Tin Hama tarehe 20 na 21 Mei, na ushiriki wao, kwa njia moja au nyingne "katika mauaji hayo
Mapigano kati ya kundi la waasi la CMA na makundi yanaounga mkono serikali ya Bamako yameendelea licha ya kusainiwa kwa mkataba wa amani mwezi Mei hadi Juni, lakini walisitisha tangu wakati huo hitimisho la "mkataba wa heshima" kati ya wadau wote katika mchakato huo Oktoba 16, baada ya wiki tatu ya mikutano katika mji wa Anefis, kaskazini-mashariki mwa Mali.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment