Image
Image

News Alert:LEMA ameibuka mshindi na kutangazwa kuwa mbunge mteule Arusha Mjini.


Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia  na Maendeleo - CHADEMA  katika Jimbo la Arusha, GODBLEES  LEMA ameibuka  mshindi  na  kutangazwa kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha  vyama  vitano  vya siasa, LEMA amepata kura Elfu-68 na 848  kati ya kura Laki-1, Elfu-4 na 353  zilizopigwa  akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Mapinduzi, PHILEMON  MOLLEL aliyepata kura  Elfu-35 na 907.
Wagombea wengine  walioshiriki  katika  uchaguzi  huo  ni pamoja na NAVO  MOLLEL wa  ACT Maendeleo  aliyepata  kura  342,  ZUBERI MWINYI  wa Chama cha Wananchi -CUF-   aliyepata  kura 106 na  MAKAMA RASHIDI  wa  NRA  aliyepata  kura  43.
Kwa mujibu wa Msimamizi  wa Uchaguzi  wa Jimbo  la Arusha,  JUMA IDDY,wapiga kura walioandishwa ni Laki-3, Elfu-17 na 814, na waliojtokeza  kupiga  kura ni Laki-1, Elfu-5 na 800.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment