Image
Image

Waziri wa kilimo,ufugaji na uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba atatua kero za wafugaji na wakulima Kagera.




Katika kuhakikisha kuwa tofauti kati ya wakulima na wafugaji nchini ambazo zimekuwa kwa muda mrefu zikisababisha machafuko zinakwisha na kubakia historia,waziri wa kilimo, ufugaji na uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amefika Mkoani Kagera,kutatua kero za wafugaji na wakulima hao.

Waziri Nchemba ambaye amelivalia njuga suala hilo na kutaka kuhakikisha kuwa mapigano kati ya wakulima na wafugaji hayajitokezi amelazimika kuongozana na Naibu waziri wa Mali Asili Mh.Ramo kwa lengo la kusaidia kuanzisha utaratibu wa kuyapitia upya mapori ya akiba ya Maswa,Kimisi,Burigi suluhisho la kudumu na pia kuhakikisha kuwa suwala la malisho kwa wafugaji linapata utatuzi wenye tija.

Pia Waziri Nchemba ametoa rai kwa wafugaji na wakulima wote kulinda maeneo ya hifadhi yaliyotengwa,Kama dhamira ya Rais John Pombe Magufuli ilivyojitoa kuhakikisha changamoto hizo zinakwisha.

Amewahakikishia wafugaji na wakulima kwamba Wizara yake kwa wakulima,Wafugaji na Wavuvi itahakikisha kuwa inamaliza na kutatua kero zao kwa kuzipatia majawabu ya kudumu hatua kwa hatua.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment