Image
Image

Miili ya wanajeshi wa KDF waliouwawa nchini Somalia yapelekwa Kenya.

Miili ya wanajeshi wa KDF waliouwawa nchini Somalia imepelekwa nchini Kenya na kupokelewa kwa heshima za kijeshi huku ikiarifiwa kwamba operesheni kubwa ya kuwakomboa wanajeshi walionusurika ikiendelea huko Somalia 
Waziri wa Ulinzi wa Kenya Raychelle Omamo alizipokea maiti za wanajeshi hao zilipowasili kwenye uwanja wa ndege jijini Nairobi huku pia kukifanyika utaratibu maalum wa kutoa heshima za kijeshi. Waziri Omamo akizungumza kwa huzuni kubwa aliwaomba wakenya waendelee kuwa na subira wakati shughuli za ukombozi wa wanajeshi zikiendelea pamoja na miili zaidi ya wanajeshi waliouwawa ikiendelea kutafutwa na kusafirishwa nchini humo.
''Huu ni wakati wa majonzi kwa jeshi la kenya na kwa taifa letu kwa ujumla.Kwa mara nyingine tungependa kusisitiza shukurani zetu kwa wakenya wanaotuunga mkono kwa upendo wao katika kipindi hiki chote kigumu kwa wanajeshi wetu na familia zao.Kama nilivyowaeleza awali shughuli ya kuwatafuta na operesheni ya uokozi zinaendelea na tunatarajia kuwapokea wanajeshi wetu zaidi kadri siku zinavyokwenda.''
Omamo hakutoa lakini idadi kamili ya wanajeshi wakenya waliouwawa ingawa ameweka wazi kwamba wanategemea maiti zaidi za wanajeshi waliowawa kusafirisha nchini kenya .Kambi ya jeshi la Umoja wa Afrika kusinimagharibi mwa Somalia ilishambuliwa na wapiganaji wa Al Shabab mapema ijumaa hili likiwa ni tukio la hivi karibuni kabisa la kikosi cha Umoja huo wa Afrika kushambuliwa ndani ya Somalia.
Hadi sasa serikali ya Kenya imekataa kusema wanajeshi wake wangapi wameuwawa,kujeruhiwa au waliotoweka lakini kundi hilo la Ashabab siku ya Jumapili lilitoa taarifa likisema zaidi ya wanajeshi 100 wakenya waliuwawa na wengine wameshikiliwa mateka.
Katika taarifa aliyoitowa rais Kenyatta amesema kundi hilo halitopata muda wa kupumua na kuahidi kwamba nchi yake italipiza kisasi ingawa haijafahamika hadi wakati huu ikiwa jeshi la kenya lililoko Somalia limeifikia kambi hiyo inayoshikiliwa na wanamgambo.
Kadhalika kundi la Al Shabab limetoa kanda mbili za sauti zilizorekodiwa likidai wanajeshi kadhaa wanashikiliwa mateka huku tovuti zao ndani ya Somalia zikidai wanajeshi 12 wanashikiliwa mateka.
 Waziri mkuu wa Somalia Omar Abdirashid Sharmake amelaani shambulizi la Alshabab akisema ni kitendo cha kinyama huku pia akitowa rambi rambi zake kwa familia za wanajeshi waliouwawa.Umoja wa Ulaya ambao ni mfadhili mkubwa a jeshi la AMISOM umelaani shambulizi hilo ukisema ni jaribio jingine la kuuhujumu mchakato wa kisiasa kuelekea somalia thabiti yenye usalama.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment