Image
Image

Shambulizi katika kambi ya jeshi la Kenya Somalia: Kenya yatikiswa.

Kenya bado iko katika hali ya sintofahamu baada ya shambulio lililosababisha vifo vya wanajeshi kadhaa katika kambi ya jeshi la Kenya nchini Somalia Ijumaa, Januari 15, wanajeshi wengi wanashukiwa kuwa bado wanashikiliwa na wapiganaji wa kundi la Al-Shebab.
Wanajeshi wengine wanashukiwa kuwa wamejificha katika maeneo jirani,wakati ambapo operesheni ya kuwaokoa imeanzishwa na jeshi la Kenya. 
Wakati huo huo,askari waliojeruhiwa na wale walionusurika wamerejeshwa katika makundi madogo mjini Nairobi.
Habari hii imegonga vichwa vya habari kwenye magazeti ya Nairobi, ambapo, manusura wameonekana kwenye picha wakishuka ndege. Jumatatu, Januari 18, askari 16 waliojeruhiwa, wakiwa hawana furaha yoyote, wamewasili nchini Kenya. Inaarifiwa kuwa askari hao waliokolewa katika kichaka nchini Somalia karibu na kambi ya El Adde siku mbili baada ya shambulizi hilo.
Upande wa jeshi, inaonekana kuwa shambulizi hilo ni pigo kubwa kwao. Mkuu wa majeshi ya Kenya, Mwathethe Samson, amefanya mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii.
"Tumeanzisha operesheni ya kuwaokoa askari wetu. Tutapambana nao kwa kina hadi katika maeneo wanakojificha, na tutaendelea hadi mwisho, kwa heshima ya kila tone la damu linalomwagika kutoka kwa ndugu zetu", Samson Mwathethe amesema.
Hakuna idadi yoyote ya askari waliouawa, kujeruhiwa au kutekwa nyara ambayo imetolewa na jeshi la Kenya, ambalo si kawaida yake ya kutoa taarifa zinazohusiana na hasara linalopata nchini Somalia. Kwa upande wake, kundi la Al-Shebab ambalo lina tabia ya kuongeza chumvi katika matokeo ya shughuli zake. Kundi hili limesema kuwa limewaua askari 121wa Kenya katika shambulio hilo.
Serikali ya Kenya kupitia Katibu Dola anayehusika na maswala ya Ulinzi Rachael Omamo, imewataka raia kuwa watulivu kufuatia tukio hilo. "Tunapaswa kudumisha umoja wetu. Tafadhali, tusitofautiane kutokana na hali hii, muwe na subira.Taarifa itatolewa mara moja ikithibitishwa.Tuko tayari kuwarejesha askari wetu nyumbani", amesema Rachael Omamo.
Kwa mujibu wa vyanzo nchini Somalia, mapigano makali bado yanaendelea katika jimbo la El Adde. Ndege za jeshi la Kenya zimeingia Somalia zikisaidiwa na askari wa nchi kavu katika jitihada za kurejesha eneo hilo, kuwaokoa wale walio mafichoni na wale ambao walikamatwa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment