Image
Image

Ban Ki-moon atarajia kuona idadi ya wakimbizi wa ndani ikipungua kwa asilimia 50.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea matumaini yake kwamba viongozi duniani watajitolea kwenye mkutano wa kilele kuhusu masuala ya kibinadamu utakaofanyika mwezi Mei huko Uturuki ili kupunguza wakimbizi wa ndani duniani angalau kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.
Kauli hiyo ameitoa alipotembelea kambi ya wakimbizi wa ndani ya Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kusisitiza kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuwa kubwa na jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuboresha misaada ya kibinadamu. Idadi ya wakimbizi wote duniani ni ndogo kuliko idadi ya wakimbizi wa ndani ambao hawajavuka mipaka kutafuta makazi na usalama.
Hadi kufikia mwaka 2014, watu milioni 38 walilazimika kukimbia makazi nchini mwao kutokana na vurugu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment