Image
Image

Mamilioni ya wananchi wa Iran wameelekea katika vituo vya kupigia kura.



Mamilioni ya wananchi wa Iran tangu mapema leo wameelekea katika vituo vya kupigia kura kuchagua wawakilishi wao katika Bunge la 10 la Jamhuri ya Kiislamu na Baraza la 5 la Wataalamu Wanaochagua Kiongozi wa Juu wa Iran.

Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu yaa Bunge la Iran lina viti 290 na Baraza la Wataalamu lina viti 88. Majlisi hizo mbili zina nafasi muhimu sana katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Bunge ndio nguzo kuu ya kutunga sheria na Baraza la Wataalamu huwa na kazi muhimu ya kumchagua Kiongozi wa Juu wa Iran.
Uchaguzi katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni dhihirisho la nguvu ya taifa, na kwa maneno ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, uchaguzi huakisi harakati adhimu ya wananchi kwa ajili ya kuimarisha zaidi utawala wa Kiislamu hapa nchini. Mahudhurio makubwa ya wananchi katika zoezi hilo daima yamekuwa kielelezo cha uhai wa mfumo wa Kiislamu. Hii leo macho ya walimwengu yameelekezwa katika uchaguzi wa Iran ambao kwa mtazamo huo ni mtihani utakaobaini kiwango cha uhalali na kushirikishwa wananchi katika maamuzi muhimu ya nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Abdul Ridha Rahmani Fazli amesema Wairani milioni 55 wametimiza masharti ya kupiga kura. Wagombea 4979 wanagombea viti 290 vya Bunge na wengine 159 wanachuana kwa ajili ya viti 88 vya Baraza la Wataalamu. Kwa msingi huo tunaweza kusema kuwa kila kiti kimoja cha Bunge kinagombewa na watu 17. Asilimia 10 ya wagombea ni wanawake.
Katika kipindi cha kabla ya chaguzi za leo za Bunge la Baraza la Wataalamu, maadui wa Jamhuri ya Kiislamu wamefanya njama za aina mbalimbali na kueneza propaganda chafu za kuwavunja moyo wananchi na kutaka kuwazuia wasishiriki kwa wingi katika zoezi hilo. Miongoni mwa mbinu zilizotumiwa na vyombo vya habari vya maadui ni kutaka kuwagawa wananchi wa Iran katika kambi mbili tofauti na kuzusha migawanyiko bandia.
Uchaguzi wa leo nchini Iran ni wa kwanza kufanyika baada ya kufikiwa makubaliano ya nyuklia na kufutwa vikwazo vya kidhalimu vya nchi za Magharibi dhidi ya Iran. Kwa msingi huo kumejitokeza maswali na uchambuzi mwingi katika duru za habari kuhusu uchaguzi wa leo hapa nchini.
Mitandao ya kijamii kama Telegram, Twitter, Facebook na Waht's app imetumiwa sana na maadui kuchambua na kutaka kuupaka madongo uchaguzi wa leo hapa nchini. Hapana shaka kuwa harakati hizo chafu za kipropaganda zinaakisi hasira za maadui wa Jamhuri ya Kiislamu kutokana na mahudhurio makubwa ya wananchi katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika hapa nchini.
Licha ya njama na propaganda hizo, tangu mapema leo mamilioni ya Wairani wameanza kutoa jibu kali kwa bwata na bwabwaja za wasiolitakia mema taifa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo la kidemokrasia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment