Image
Image

Rais wa Yemen,amemteua kamanda mkuu msaidizi wa jeshi nchini humo.


Rais Abd Rabbu Mansour Hadi wa Yemen, amemteua kamanda mkuu msaidizi wa jeshi ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuutwaa tena mji wa Sanaa kutoka kwa waasi. Rais Mansour amemteua Jenerali Ali Al Ahmar na kumwapisha mjini Riyadh huku akiahidi kutwaa tena mji wa Sanaa.
Jenerali Al Ahmar aliasi jeshi la serikali na mwaka 2011 alijiunga na harakati za kumwondoa madarakani aliyekuwa rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh.
Maofisa walio karibu na Rais Hadi wanasema hatua hiyo inalenga kutafuta uungaji mkono wa makabila yenye silaha yanayomtii Jenerali Al Ahmar, dhidi ya waasi.
Waasi wanaoungwa mkono na Iran na wapiganaji wanaomtii aliyekuwa Rais wa nchi Bw Saleh, walitwaa udhibiti wa mji wa Sanaa mwezi Septemba mwaka 2014

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment