Image
Image

Serikali yasisitiza azma yake ya kupambana na mafisadi na walarushwa nchini Tanzania.


Serikali ya Tanzania ya awamu ya tano imesema kuwa bado itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi hadi itakapo jiridhisha kwamba vitendo hivyo vimekwisha na nchi inakwenda katika mstari ulionyooka ili kuweka usawa kwa walionacho na wasio nacho.
Kauli hiyo ameitoa Waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya maadili kwa mawaziri na manaibu waziri jijini Dar es Salaam.
Mhe.Majaliwa amesema vitendo vya rushwa na ufisadi vinatia hasara serikali ya mamilioni ya fedha ambazo zingeweza kutumika kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi na kusisitiza tatizo hilo linaweza kupungua iwapo viongozi watazingatia sheria ya maadili.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment