Image
Image

Wanao jinufaisha kupitia vituo vya watoto yatima watangaziwa kiama.

Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha imetangaza kuanza kuvifunga vituo vyote vya kulelea watoto ambavyo wamiliki wake wanatumia fursa hiyo kujinufaisha.
MKUU wa Wilaya ya Arumeru Wilson Ngambaku amesema  Serikali inapitia usajili wa vituo hivyo pamoja na kuangalia utendaji kazi wake na kwamba vituo vyote ambavyo vinafanyakazi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi vitafutiwa usajili wake mara moja.
Nkambaku ametoa kauli hiyo wakati yeye pamoja na wanachama wa Chama cha mapinduzi walipotembelea kituo kimoja cha yatima ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya CCM ambapo kwa mkoa wa Arusha yamefanyika katika kata ya Ngarenanyuki Wilayani Arumeru
Katika maadhimisho hayo wanachama wa chama cha mapinduzi Mkoani Arusha wametumia fursa hiyo kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ambapo  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Bernad Murunya amesema ni vyema sasa wanachama kuondoa makundi na kuzidi kukijenga chama hicho ambacho amekitaja kuwa mfano wa kuigwa ndani ya bara la Afrika
Shughuli nzote hizo zinaafanyika wakati huu ambapo chama tawala cha mapinduzi CCM ambacho ni zao la vyama vya TANU na ASP kinaadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment