Image
Image

9 walazwa kwa kula samaki wenye vimelea vya Kipindupindu Lindi.



Watu tisa wamelazwa katika zahanati ya Mpekenyela wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi baada ya kula samaki wanaosadikiwa kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Kipindupindu na kuwasababishia kuhara na kutapika na  kupoteza nguvu.
Kufuatia tukio hilo wafanyabiashara wawili wa Samaki katika kata ya Mpekenyela na Namungo wilaya ya Ruangwa Somoe Kishoka na Fatuma Saidi wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuuza samaki wenye vimelea vya Kipindupindu.
Akizungumzia tukio hilo mganga mfawidhi wa zahanati ya Mpekenyela Mikidad Mbule  anathibitisha kupokea wagonjwa hao,huku ndugu wa mgonjwa aliyelazwa  kutokana  na maambukizi anaelezea hali hiyo ilivyomkuta . 

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment