Image
Image

Latest News:Wabunge 3 wanaotuhumiwa kwa Rushwa waburuzwa Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini TAKUKURU imewafikisha Mahakama ya Kisutu  Jijini Dar es Salaam wabunge watatu walio katika kamati  za Bunge kwa tuhuma za Rushwa.
Miongoni mwa wabunge hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,Mh.Victor Mwambalaswa Mbunge wa Lupa,Sadick Murad Mbunge wa Mvomero na Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara.
Wabunge hao sasa wanakamilisha taratibu za dhamana kwa kila mmoja kulipa shilingi Million 5 na watakua nje hadi April 15 kesi yao itakapo sikilizwa tena.
Hata hivyo kwa siku kadhaa za nyuma vuguvugu lilitanda juu ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hali iliyo lazimu kujiuzulu kwa Baadhi ya wabunge.
Kutokana na shutuma za Rushwa miongoni mwa wabunge akiwamo Mbunge wa Nzega Mjini na Kiongozi wa chama cha CCM,aliishtumu Kamati ya Huduma za Jamii anayohudumu kuwa kuna baadhi ya Wajumbe walipokea rushwa na kuchukua uamuzi wa kuungana  na  Mh.Zitto Kabwe,kumuandikia barua Spika wa Bunge ya kujiuzulu  na kumtaka achunguze na kuchukua hatua.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment