Image
Image

Marekani yasitisha ufadhili wake kwa Tanzania likilalamikia matukio ya uchaguzi wa Zanzibar na upitishwaji sheria ya Mtandao.

Shirika la ufadhili la serikali ya Marekani limesitisha ufadhili wake kwa serikali ya Tanzania likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea ufadhili wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.
Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema: "Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”
Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao "haukujumuisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.”
Mabalozi wakosoa uchaguzi wa Zanzibar
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Chama cha Wananchi (CUF).
MCC imesema kwamba huwa inatilia mkazo sana demokrasia na kujitolea kwa nchi kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.
"Uchaguzi uliofanyika Zanzibar na kutekelezwa nwa Sheria ya Uhalifu wa Mitandao vinaenda kinyume na hili,” imesema.

Tanzania ilipokea Dola 698 milioni katika awamu ya kwanza.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment