Image
Image

Tanzania na Uganda zaanza mchakato wa ujenzi wa bomba la Mafuta utakao gharimu dola za marekani Bilioni 4.


Tanzania na Uganda zimeanza mchakato wa utekelezaji wa mradi wa  ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka katika nchi ya Uganda  hadi  bandari ya Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kugharimu dola  za  Kimarekani bilioni nne.
Makubaliano ya kujengwa kwa mradi huo yalifikiwa na marais wa nchi  hizo  Dr,John Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda   walipokutana  jijini Arusha wakati wa kikao  cha wakuu wa nchi za  jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mawaziri wa sekta zinazohusiana na nishati,makatibu wakuu na  watendaji wa ngazi mbalimbali wa  nchi za Tanzania na Uganda  wamekutana jijini Arusha na kusaini makubaliano ya kuanza  kwa  mchakato ambao waziri wa nishati wa Uganda Bi.Irine Liuloni  amesema mradi huo utaongeza chachu ya uchumi kwa nchi za Afrika  Mashariki .
Aidha viongozi hao wamesema kitakachofuata baada ya hatua hiyo ni  taratibu za  ndani za serikali za Tanzania na Uganda na kwamba mradi  huo unaotekelezwa na kampuni ya kimataifa ya uchimbaji wa mafuta  ya total unatarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa mwaka 2017.
Kama mradi huo utakamilika na kuanza uzalishaji unatarajiwa  kuongeza fursa za kiuchumi na ajira kwa wananchi wa nchi za Jumuiya  ya Afrika Mashariki.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment