Image
Image

Tukio la kutekwa Mwanahabari lalaaniwa vikali kila kona*polisi wapewa muda kutafuta alipo.

Wanaharakati wa haki za binaadamu na jumuiya za waandishi wa habari nchini Tanzania wametoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa mwandishi wa habari wa magazeti ya Mwananchi Communications na mwakilishi wa Deutsche Welle visiwani Zanzibar, Salma Said, ambaye ametoweka tangu jana katika mazingira ya kutatanisha.
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC) umesema unapingana na kitendo hicho ambacho umesema kinarejesha nyuma jitihada za waandishi kufanya kazi zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan, ameiambia DW kwa njia ya simu kwamba kukamatwa kwa Salma katika mazingira yasiyoeleweka ni hatari kwa uhuru wa habari. "Huku ni kumtisha ili asifanye kazi yake ya uandishi kwa haki na uadilifu na haikubaliki. Serikali inaonekana kutumia nguvu sana dhidi ya waandishi kama yeye na hivyo si sawa. Tutasimama pamoja naye na tunataka aachiliwe mara moja."
Katika ujumbe wake, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binaadamu nchini humo (THRD) umesema kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa unalaani vikali kutekwa kwa mwandishi huyo wa kike na kuvitolea wito vyombo vya usalama "kutoa ushirikiano katika kipindi hiki" na pia kuwataka waandishi wa habari "kuungana ili kushinikiza" apatikane haraka.
Salma Said mwenye umri wa miaka 45 alitoweka jana visiwani Zanzibar katika mazingira ya kutatanisha na hadi sasa bado familia yake haijui alipo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment