Image
Image

Watumishi watatu jeshi la Zima moto watumbuliwa kwa wizi wa mafuta ya Ndege na mizigo ya wateja DSM.

Saidi Msangi,Dar es Salaam.
Serikali imewasimamisha kazi maafisa 3 wa jeshi la kikosi cha zimamoto kwa tuhuma za kushiriki wizi wa mafuta ya ndege na mmoja kati yao kuiba mizigo ya wateja kwa kushirikiana na wafanyakazi wa kampuni ya swissport.
Akizungumza katika ziara ya kushitukiza aliyoifanya katika viwanja vya ndege vya Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam naibu waziri wa wizara ya mambo ya ndani Mhe.handisi Hamad Masauni amewataja walio simamishwa kazi ni ALFANI KISANA na MUSSA MANDAULI ambao walikamatwa na madumu 10 ya mafuta ya ndege wakiwa na gari la serikali lenye usajiri STJ 2948 huku askali mwingine aliye julikana kwa jina la ABIAS Mwanza akishutumiwa kwa kosa la kushirikiana na mfanyakazi wa swissport lucas maganda kwa kosa la kuiba mzigo abiria.
Akiwa katika kiwanja hicho Mhe.Masauni amekagua utendaji kazi katika idara ya uhamiaji,polisi na jeshi la zimamoto na kuagiza viongozo wa idara hizo zilizopo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa uaminifu na yeyote atakaye kiuka atua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment