Image
Image

Siri Nzito ya utumbuaji Majipu ya Rais Magufuli yabainika.

            Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.
Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
ALIYEKUWA Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amefichua siri ya Rais Dk. John Magufuli kutumbua majipu kwa kasi, tangu ameingia madarakani mwaka jana.
Akizungumza wakati wa kuzindua ripoti mbili za Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi na Mafuta (TEITI), mjini Dar es Salaam jana, Utouh alisema akiwa CAG aliandaa ripoti nyingi  ambazo utawala uliopita haukizifanyia kazi.
Alisema Rais Magufuli anatumia ripoti hizo kutumbua vigogo mbalimbali, kwa sababu amekuta mambo yako mezani.
“Ripoti zangu nikiwa CAG ndizo zinasomwa bungeni, zimeonyesha udhaifu maeneo mbalimbali ya taasisi za Serikali na nyingine.
“Nyingi zilikabidhiwa zamani,viongozi waliopita hawakuzifanyia kazi…nawaambua utumbuaji majipu unaofanywa  na Rais Magufuli, utasaidia kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato na nidhamu sehemu za kazi.
Alisema ni jukumu la kila mwananchi kulinda rasilimali zilizopo na kwa kufanya hivyo, mapato yataongezeka.
Kuhusu sheria ya madini iliyopitishwa mwaka jana, inayozungumzia uwazi na uwajibikaji katika sekta ya madini, Utouh alisema imesaidia kuleta nidhamu katika sekta hiyo, kwa sababu kabla ya hapo mapato mengi yalikuwa yakipotea.
Naye Mwenyekiti wa TEITI, Jaji Mark Bomani alisema taarifa za kazi za TEITI katika ripoti ya mwaka 2013/14, zim
esaidia kunufaisha uhamasishaji uwazi katika sekta ya madini nchini.
Alisema sekta hiyo ilianza kushamiri mwaka 1990,  haikuwa na manufaa kwa uchumi wa nchi kwa vile mapato kwa Serikali hayakuwa wazi.
Alisema mwaka 2007, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete aliunda kamati ya kuchunguza sekta ya madini ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ikilalamikiwa na wadau wengi.
Alisema  upotevu wa fedha
za Serikali mwaka 2009, zilikuwa hazionekani, lakini CAG Utouh alifanya ukaguzi ambao umesaidia fedha za madini kuongezeka.
“Ripoti ya mwaka 2014 inaonyesha pato katika sekta hii, limeongezeka kwa asilimia 10…takwimu zetu zinaonyesha awali kampuni za madini zilikuwa 11, sasa zimefika 60 zikiwamo kubwa na za kati,”alisema.
Utouh alistaafu rasmi kazi S
eptemba 2014, baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka saba alipoteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2006.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment