Image
Image

Korea Kaskazini yakanusha pendekezo la Donal Trump kufanya mazungumzo kuhusu silaha za nyuklia.

So Se Pyong balozi wa korea kaskazini katika bazara la Umoja wa Mataifa mjini Geneva alizungumza ya kwamba serekali ya Korea Kaskazini haina wazo wala fikra ya kufanya mazungumzo na yeyote.
So Se Pyong alindelea kusema ya kwamba kauli ya Donald Trump mgombea wa kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha Republican nchini Marekani   ameyasema hayo kwa kutaka kujifanyia kampeni na kauli ya mgombea huyo ni kauli isio kuwa na maana.
So Se Pyong aliyazungumza hayo katika mahojiano na shirika la habari la Reuters la nchini uingereza hiyo jana katika kongamano la  kwanza la chama tawala cha nchini Korea Kaskazini  mjini Pyongyang Korea kaskazini.
Ifahamahike ya kwamba kauli hiyo ya So Se Pyong  ilitokana na kauli ya Donald Trump wiki iliopita baada ya mgombea huyo kuzungumza ya kwamba ikiwa atafaanikiwa kuwa rais wa Marekani ataanzisha mazungumzo baina ya Marekani na Korea Kaskazini ili kuishawishi nchi hiyo kuachana na mpango wake wakuendelea na zoezi la kutengeneza silaha za nyuklia. 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment