Image
Image

Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman katika nyanja mbalimbali kwa faida ya nchi zote mbili.
Mheshimiwa Samia ameyasema hayo leo alipokutana na Balozi wa Oman anayemaliza muda wake nchini Saud Ali Mohamed Al-ruqaishi ambaye alifika ofisini kwake Ikulu kwa ajili ya kumuaga.
"Sisi Tanzania tunajua tuna wajibu wa kukuza uhusiano na Oman, uhusiano wetu siyo wa kibalozi tu, umeota mizizi, kwani ni wa muda mrefu na ni wa kindugu," alisema Makamu wa Rais.
Alibainisha kuwa serikali imekuwa na uhusiano na Oman katika nyanja za elimu na hasa elimu ya juu ambapo Oman imesaidia katika ujenzi wa Chuo cha Afya, Mbweni  na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar.
Aidha, alisema serikali ya Oman imeanzisha Mfuko Maalum ikiwa ni ufadhili kwa wanafunzi wa Zanzibar  katika elimu ya juu pamoja na kukijengea uwezo Chuo  Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.
Pamoja na misaada hiyo Makamu wa Rais aliiomba serikali ya Oman kuangalia  uwezekano wa uwekezaji katika sekta za kilimo na biashara ambako kuna fursa nyingi za uwekezaji.
Katika mazungumzo hayo Balozi Al-ruqaishi alitoa shukrani zake kwa serikali ya Tanzania kutokana na ushirikiano aliopatiwa katika kipindi chote alichokuwepo nchini jambo ambalo limwemwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment