Image
Image

Walioua ndani ya msikiti tunawajua.

KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, amesema jeshi lake tayari linawafahamu watuhumiwa wote waliohusika na mauaji ya watu watatu msikitini.
Aidha, Msangi alisema msako mkali unaendelea ili kuwakamata watu waliomuua Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bulale, Alphonce Mussa mapema wiki hii.
Akizungumza na Nipashe jana, Kamanda Msangi alisema msako uliofanywa na jeshi lake akiwa miongoni mwao, ulifanikisha kukamata watu 14 wakiwamo waliohusika moja kwa moja na mauaji ya watu watatu katika Msikiti wa Rahmani Ibanda Relini kata ya Mkolani, akiwamo Imamu Feruzi Elias.
Wengine waliouawa kwa kuchinjwa katika msikiti huo, Mei 18, mwaka huu, saa 3:00 usiku, Mbwana Rajab na Khamis Mponda, ambao walikuwa wakiswali kabla ya kuvamiwa na wauaji hao.
“Lengo la kuwasaka watu hawa ni kutaka kuiweka Mwanza katika hali ya usalama zaidi, ili kila mtu aweze kuishi kwa amani na utulivu…wananchi lazima wajue kazi inafanyika kwa usahihi,” alisema Kamanda Msangi.
Aidha, Msangi alisema bado polisi wanaendelea na uchunguzi wa mauaji yaliyofanyika Jumapili iliyopita katika mtaa wa Bulale kata ya Buhongwa, kutokana na mauaji hayo kutokuwa na viashiria vya ujambazi.
Alisema waliohusika na mauaji hayo ya Mwenyekiti Mussa, taarifa zitatolewa kupitia vyombo vya habari kabla ya kuwafikisha vyombo vya sheria.
Hata hivyo, Kamanda Msangi alisema katika mauaji yaliyotokea wiki mbili zilizopita wilayani Sengerema na kuhusisha kaya moja ya watu saba, polisi ilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote.
“Hawa waliokamatwa Sengerena kwa mauaji ya watu saba, baadhi yao ni ndugu ambao walikutwa na vithibitisho vya marehemu zikiwamo simu za mkononi,” alisema.
    Share on Google Plus

    Kuhusu TAMBARARE HALISI

    This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

    0 comments:

    Post a Comment