Image
Image

Merkel aionya Uingereza: Hakuna faida bila uwajibikaji.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameionya Uingereza isitarajia kuendelea kupata faida ilizokuwa ikizipata katika Umoja wa Ulaya, hata baada ya kuamua kujitenga na Umoja huo.
Akizungumza katika mkutano maalum mjini Berlin kabla ya kwenda Brussels kushiriki katika mkutano wa wakuu wa Umoja wa Ulaya, Bi Merkel amesema ukijiondoa katika familia, huwezi kuendelea kunufaika bila kuwajibika.
Merkel amesisitiza kuwa hayatakuwepo mazungumzo yoyote na Uingereza, yawe rasmi au vinginevyo, kabla ya nchi hiyo kuwasilisha ombi la kujiondoa katika Umoja huo.
Bi Merkel amesema kujiondoa kwa Uingereza, maarufu kama Brexit, hakuwezi kuipotosha Ulaya katika kushughulikia changamoto kubwa zilizopo. Mkutano wa Brussels unajadili hatua ya Uingereza kuondoa uanachama wake katika Umoja wa Ulaya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment