Image
Image

Polisi ya Uturuki imeendesha operesheni dhidi ya makundi yanayoshukiwa kuwa ya Dola la Kiislamu.

Polisi ya Uturuki imeendesha operesheni dhidi ya makundi yanayoshukiwa kuwa ya Dola la Kiislamu mjini Istanbul na mji wa pwani ya bahari ya Aegean wa Izmir, siku mbili baada ya mashambulizi matatu ya kujitoa muhanga yaliyouwa watu 42 katika uwanja wa ndege wa Istanbul. Polisi wa kupambana na ugaidi wakiongozwa na vikosi maalumu wamefanya uvamizi katika maeneo matatu yanayokaliwa na wafanyakazi mjini Istanbul - limesema shirika la habari la serikali Anadolu bila kutaja vyanzo vyake. Wakati huo washukiwa tisa wanaodhaniwa kuwasiliana na wanachama wa kundi la IS nchini Syria, walikamatwa katika uvamizi katika wilaya tatu za Izmir, wakituhumiwa kwa kufadhili, kuandikisha na kutoa msaada wa usafiri kwa kundi hilo la itikadi kali. Awali vikosi vya usalama vimeripotiwa kuwauwa washukiwa wawili wa Dola la Kiislamu kwenye mpaka wa Syria, ambao inaamiwa walikuwa wanapanga njama ya kufanya mashambulizi ya kujitoa muhanga nchini Uturuki.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment