Image
Image

Kagame azitaka nchi za Afrika Mashariki kuzalisha bidhaa zilizobora.

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema nchi za Afrika ya Mashariki zinapaswa kujizatiti katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora ili kuinua soko la bidhaa zinazozalishwa katika ukanda huo na kuzifanya zipate soko nje ya nchi hizo.
Rais Kagame amesema hayo wakati akifungua maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere na kuongeza kuwa uwezo wa kuzalishwa bidhaa bora katika ukanda wa nchi za Afrika ya Mashariki upo.
Naye rais wa Tanzania Mhe.Dr.John Pombe Magufuli amesema ataendelea kuhimiza wakazi wa nchi za Afrika ya Mashariki umuhimu wa nchi zao kuwa vinara wa uzalishaji wa bidhaa za ndani ili kuimarisha uchumi wa nchi zao.
Ufunguzi rasmi wa maonesho hayo ya 40 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaaam umeenda sambamba na kutoa zawadi kwa mabanda ambayo yamefanya vizuri kwa mwaka huu.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment