Image
Image

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.

Bw. Joseph Odo Haule - Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Dkt. James Munanka Wanyancha.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa leo Mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo tarehe 28 Julai, 2016.
Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.
Uteuzi wa Bw. Joseph Odo Haule umeanza leo tarehe 28 Julai, 2016.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Joseph Odo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara (Road Fund).
Wajumbe wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi zao.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment