Image
Image

TANZIA:Mpiga picha ya Marehemu Mwangosi,Joseph Senga Afariki Dunia.

Daudi Mwangosi akishambuliwa na askari polisi - Picha iliyopigwa na Marehemu Senga wa Gazeti la Tanzania Daima 2012.
Taarifa zilizotufikia zinadai kuwa mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Mwandishi wa Habari wa kituo cha Channel Ten Daudi ya Mwangosi amefariki dunia.
Taarifa hizo zenye kushtua wanataaluma ya habari pamoja na watu wengine zinajiri ikiwa ni siku moja tu pale ambapo MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa, KUmhukumu kwenda jela miaka 15 askari polisi Pasificus Simon, kwa kumuua bila kukusudia aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi, huku picha aliyoipiga Marehemu Senga ikiwa ndio imeendelea kutumika katika ushaidi juu ya mauaji ya Mwangosi.
Mwangosi aliuawa Septemba 2, 2012 eneo la Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa, baada ya askari kuzuia mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
huku picha pekee ya tukio hilo iliyosambaa ulimweenguni kote ikiwa iliyopigwa na Jemedari
JOSEPH SENGA aliyekuwa mpiga picha wa gazeti la Tanzania DAIMA.

 "Mwandishi Nguli nchini Tanzania Dotto Bulendu ameandika taarifa hii katika ukurasa wake wa Facebook:
"Simanzi,siku moja baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kumfunga miaka kumi na mitano askari ya aliyemuua Daudi Mwangosi,tasnia ya habari yapata pigo,mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi ya Mwangosi,SHUJAA JOSEPH SENGA,amefariki dunia usiku huu.
Senga amefia nchini India alikopelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo.
Bila Joseph Senga,shujaa aliyehatarisha maisha yake,akasimama bila woga,akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi wenye silaha,huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi,milio ya risasi ikisikika,na kuzitunza,zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi,leo hii asingekuwa Senga,nadhani kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu dhidi ya aliyemuua Mwangosi.Nakulilia Senga..
Senga,Senga,Senga,Senga,umekwenda,Mungu aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho amekuchukua,Senga umekwenda wadogo zako katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.
Senga,Senga,kamsalimie Daudi Mwangosi,mwabie aliyemuua nae kahukumiwa jela miaka 15,kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu.
Nenda Senga,picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi"
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment