Image
Image

UTAFITI:Kukaa kwa muda mrefu sehemu za kufanyia kazi husababisha kisukari.

KUNA sababu nyingi za kuacha kukaa na badala yake mtu kufanya kazi akiwa amesimama. Lakini kupunguza uzito pengine si moja kati ya hizo, kwa mujibu wa utafiti mpya ambao umepima kwa usahihi kiasi cha kalori ambacho watu hupunguza wakati wa shughuli za kila siku za ofisini.

Matokeo ya utafiti huo mpya yanaonyesha kufanya mara nyingi kitendo cha aina moja wakati mtu akiwa kazini huweza kutusaidia kuepuka kuongezeka uzito.
Lakini kitendo hicho cha aina moja si kusimama.
Wengi wetu hukaa zaidi kuliko kusimama, na muda wetu mwingi wa kukaa hutumika kazini, kwa sababu kazi nyingi za siku hizi ni za kukaa.
Wengi wetu hutumia saa sita mpaka saba tukiwa kwenye meza zetu kila siku.
Muda huu mwingi, wa kutoshughulisha miili umehusishwa na ongezeko la hatari ya kupata kisukari, ugonjwa wa moyo, vifo vya haraka na, lakini muhimu pia, kuongezeka uzito.
Katika kupambana na hilo, wengi wetu, nikiwemo mimi, tumeanza kutafuta njia za kupunguza muda wa kukaa. Tumepakua 'apps' kwenye smartphone zetu ambazo hutukumbusha kusimama mara kadhaa ndani ya saa moja.
Mabosi wenye kuzingatia afya wameandaa mikutano ya kutembea, ambapo wafanyakazi hujadiliana masuala ya kazi huku wakitembea kwenye kumbi. Na meza za kusimama zimekuwa maarufu.
Utafiti uliofanyika hivi karibuni umeonyeha kuwa maamuzi ambayo hutuinua kwenye viti vyetu yanaweza kutusaidia kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu na kupunguza hatari ya kupata kisukari na magonjwa sugu. Lakini cha msingi zaidi hali halisi ni kinyume kwani wengi wetu tunainuka kwenye viti kwa matarajio kuwa kukaa muda mfupi kutasaidia kutonenepeana.
Katika hali ya kushangaza tafiti chache, hata hivyo, zimefuatilia kwa karibu kiasi cha ziada cha kalori ambacho hupungua kama tutasimama ama kutembea tembea katika ofisi zetu.
Hivyo katika utafiti mpya, ambao ulichapishwa katika jarida la mwezi huu la 'Journal of Physical Activity and Health' (Jarida la Mwili Kujishughulisha na Afya), watafiti katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh, hapa Marekani walikusanya watu 74 wenye afya zao waliojitolea. Wengi wlaikuwa katika umri wa miaka ya katikati mwa 20, wa uzito wa kawaida, na wenye uzefu wa maisha ya ofisini.
Watu hawa, bila ya utaratibu maalumu, walipangwa katika makundi manne. Kundi moja lilitakiwa kukaa na kuchapa katika kompyuta kwa dakika 15 na kisha kusimama kwa dakika 15, kisha kuzunguka zunguka ofisini humo.
Kundi lingine lilikaa kwa dakika 15, lakini liliangalia televisheni bila ya kupiga chapa kwenye kompyuta. Baadaye, wakahamia kwenye mashine ya mazoezi haraka na kutembea kwa dakika 15 kwa mwendo wa pole.
Kundi la tatu lilisimama kwa dakika 15 kisha likakaa chini kwa dakika 15.

Na kundi la mwisho lilitembea kwenye mashine ya mazoezi kwa dakika 15 kisha kukaa.
Wakati wote, watu hao walivaa vifunika uso ambavyo vilirekodi kiasi cha nguvu wanchotumia, kitu kinachomaanisha kiasi gani cha kalori wanapoteza.
Kama ilivyotarajiwa, kukaa hakukuchukua kiasi kikubwa. Watu hao wlaipoteza kalori 20 katika dakika 15 za kukaa, iwe walikuwa wakipiga chapa kwenye kompyuta au kutazama televisheni.
Kama ilivyotarajiwa zaidi, kusimama hakukuwa na tofauti sana. Wakiwa wamesimama kwa dakika 15, watu hao walipoteza kalori mbili zaidi kulinganisha na wakati walipokuwa wamekaa. Haikujalisha kama walikaa kisha wakasimama ama walikaa kisha wakasimama. Kiasi cha kalori walichotumia kilikuwa kama kilicholingana na hakikuwa kikubwa.
Kwa ujumla, ni kwamba, watafiti waliamua, mtu aliyesiama akiwa kazini badala ya kukaa atapoteza kalori nane mpaka tisa zaidi kwa saa.
(Kwa ajili ya kupata picha halisi, kikombe kimoja cha kahawa ya maziwa na sukari kina kalori 50.)
Lakini kutembea ilikuwa habari nyingine.

Wakati watu hao walipotembea kwa dakika 15, hata taratibu tu, walipoteza mara tatu ya kalori kulinganisha na wakati walipokuwa wamekaa au kusimama.
Kama wangetembea kwa saa moja, watafiti walipiga hesabu, wangepoteza kalori 130 zaidi kama wangekuwa wamekaa kwenye viti vyao ama kusimama kwenye madawati yao, matumizi ya ziada ya kalori ambayo yangetosha, wameandika, kusaidia watu kuepuka ongezeko hatari la uzito wa mwili la kila mwaka.
Hitimisho la utafiti ni kwamba kama lengo lako kazini ni kudhibiti uzito wako, basi “kusimama kunaweza kusitoshe,” anasema Seth Creasy, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Pittsburgh na muandishi mkuu wa utafiti huo mpya.
Utatakiwa pengine kujumuisha pia kutembea katika matendo yako ya kazini, anasema. Pengine “weka printa kwenye chumba kingine cha mbali, au simama uende kwenye friji la maji kila baada ya saa hivi” badala ya kuweka chupa ya maji kwenye meza yako.
“Dakika chache za kutembea zinaweza kujumlishwa na kuleta tofauti kubwa” katika matumizi ya kalori, alisema, wakati kusimama hakuchomi kalori 'kihivyo'.
Ni kweli, kusimama kuna faida nyingine kiafya mbali na kudhibiti uzito wa mwili, Creasy alisema, ikiwemo udhibiti bora wa sukari ya damu na upungufu wa maumivu ya mgongo na kiuno yanayohusishwa na kukaa kutwa nzima kwenye kiti.
Hivyo usivunje wala kutupa tabia ya kusimama kwa kusimama. Lakini usiitegemee kukusaidia kuondoa sukari uliyobugia kwa njia ya chakula kwenye mlo wa mchana.
New York Times
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment