Image
Image

Haya ndio matatizo ambayo huchangia baadhi ya wanawake kushindwa kushika mimba kirahisi

Tatizo la uvimbe kwenye mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama 'fibroid.' Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.

Tatizo hili linawakuta wanawake wengi hasa walio katika umri wa miaka ya uzazi, kimsingi tatizo hili limekuwa likishuhudiwa na watu wengi pengine kutokana na watu wanavyoishi.

Tatizo hili pia huwa na dalili zake na miongoni mwa dalili hizo ni pamoja na kuhisi maumivu ya kiuno hasa wakati wa hedhi, kupata maumivu makali ya tumbo na kuhisi maumivu waati wa tendo la ndoa.

Dalili nyinyingine ni kutokwa damu isiyo ya kawaida wakati wa hedhi na zisizokuwa na mpango, kuhisi maumivu ya mgongo na kupata haja ndogo mara kwa mara kutokana na uvimbe kukandamiza kibofu cha mkojo.

Mbali na dalili hizo pia dalili nyingine ni pamoja na kutotunga mimba au mimba kuharibika na kutoka, na wakati mwingine ugumba.

 
Tatizo hili la uvimbe kwenye mfuko wa uzazi 'fibroids' huweza kusababisha mwanamke kushindwa kupata mtoto kwasababu uvimbe huu unapokuwa sana hukandamiza mirija ya kupitisha mayai kutoka kwenye ovari au sehemu mayai yanapotengenezwa. Uvimbe huu pia unaweza kuzuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi. Pia hufanya mfuko wa kizazi ukaze na hivyo kushindwa kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai.
Tunapaswa kujua kuwa wanawake wengi wana 'fibroids' ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina dalili ni ngumu kufahamu. Kwa mantiki hiyo tunashauriwa kuwa na mazoea ya kufanya uchunguzi wa afya zetu mara kwa mara ili kuweza kushughulikia haraka matatizo kama haya.

Moja ya matatizo ambayo huleta huzuni na uchungu ndani ya familia ni pamoja na hili swala la familia kushindwa kubahatika kupata watoto.

Hali hiyo hupelekea huzuni ndani ya nyumba, chuki, lawama, kejeli na kushutumiana na kusababisha hata talaka pia kati ya wanandoa

Lakini leo nimeona nianze kuzungumzia hili tatizo la kuziba kwa mirija ya uzazi jambo ambalo mwishowe hupelekea ugumu wa mama kushika ujauzito.

Matatizo ya kuziba mirija hutokea pale mwanamke anapopata maambukizi ya mara kwa mara ukeni yanayoambatana na muwasho kutokwa na uchafu na usaha ukeni, maumivu wakati wa tendo la ndoa na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.

Maambukizi hayo huwa na nafasi kubwa ya kusababisha mirija kuziba na ikiwa nje ya mirija husababisha mirija kujikunja.

Maambukizi haya yasipotibiwa kikamilifu huenea hadi katika mfuko wa uzazi na kushambulia tabaka la ndani la kizazi na kusababisha tatizo liitwalo ‘Endometriosis’ ambapo mwanamke hulalamika maumivu ya chini ya tumbo au chini ya kitovu mara kwa mara, kutokwa na uchafu ukeni na dalili nyingine zenye kufanana na hizo.

Dalili ambazo huashiria mwanamke tayari amepatwa na tatizo hili la mirija kuziba ni pamoja na mwanamke kutafuta ujauzito kipindi kirefu bila mafanikio.

Pia mwanamke mwenye shida hii mara nyingi huwa na kawaidia ya kupatwa na maumivu chini ya tumbo kwa muda mrefu.

Dalili nyingine ni kuharibika kwa mimba mara kwa mara au kuzaa mtoto mmoja kisha unapotafuta mwingine huwa inakuwa ni kazi ngumu kumpata tena.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment