Image
Image

Kiongozi wa Boko Haram Nigeria, Aboubakar Shekau ajeruhiwa kwenye shambulio nchini humo.

Kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria Aboubakar Shekau amejeruhiwa vibaya kwenye shambulio la angani lililotekelezwa na jeshi la nchi hiyo, taarifa ya jeshi imesema.
Makamanda wengine wakuu wa kundi hilo pia wameuawa.
Taarifa kutoka kwa jeshi la angani la Nigeria imesema shambulio hilo lilitekelezwa Ijumaa tarehe 19 Agosti viongozi hao walipokuwa wakishiriki sala ya Ijumaa katika kijiji cha Taye, eneo la Gombale katika msitu wa Sambisa jimbo la Borno.
Kwa mujibu wa jeshi, makamanda ambao wameuawa ni pamoja na Abubakar Mubi, Malam Nuhu na Malam Hamman.
"Kiongozi wao, anayefahamika kama, "Abubakar Shekau", anaaminika kujeruhiwa vibaya begani," jeshi limesema kupitia taarifa iliyotolewa na naibu mkuu wa mawasiliano Kanali Sani Kukasheka Usman.
Kundi la Boko Haram karibuni limekabiliwa na mzozo wa uongozi.
Kundi la Islamic State lilitangaza kwamba Abu Musab al-Barnawi ndiye kiongozi mpya wa Boko Haram.
Lakini muda mfupi baadaye, Shekau alisema kuwa bado ndiye anayeliongoza kundi hilo na akamshtumu al-Barnawi kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi yake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment