Image
Image

Serena Williams kuweka rekodi ya 23 US Open.

BINGWA wa mchezo wa tenisi nchini Marekani, Serena Williams, anatarajia kuweka rekodi ya 23 katika michuano mikubwa ya Grand Slam katika US Open. Nyota huyo alishindwa kushiriki michuano ya Cincinnati wiki iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya bega baada ya kurudi katika michuano ya Olimpiki nchini Brazil.
Mbali na kusumbuliwa na maumivu hayo, kocha wake, Patrick Mouratoglou, amedai kuwa nyota huyo bado bega lake alijawa sawa kwa asilimia 100, lakini anaweza kucheza michuano hii ya US Open na kuweka historia.
Bingwa huyo namba moja kwa ubora duniani kwa upande wa wanawake, anatarajia kushuka dimbani leo dhidi ya mpinzani wake kutoka nchini Urusi, Ekaterina Makarova, huku kocha huyo akidai kuwa maumivu ya Serena si makubwa na hayawezi kumsumbua.
“Maumivu ya Serena ndani ya siku hizi chache yametulia, ni wazi kwamba bega hilo halijakamilika kwa asilimia 100, lakini bado kidogo sana kupona, hivyo kwa sasa yupo katika hali zuri ya kupambana.
“Alikwenda kushiriki michuano ya Olimpiki nchini Brazil lakini bega lilimfanya ashindwe kufanya vizuri, nguvu zake anazimalizia kwenye michuano hii ya US Open,” alisema Mouratoglou
Serena alifanikiwa kufanya vizuri katika michuano ya Wimbledon mwezi uliopita na kutwaa taji hilo alipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika michuano ya Olimpiki lakini aliyaaga mashindano hayo mapema.
Tangu atolewe kwenye michuano hiyo ya Olimpiki, hadi sasa hajafanikiwa kushuka dimbani, lakini leo ataonesha uwezo wake katika US Open.
 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment