Image
Image

Star Times lawamani kwa kutoza malipo chaneli za bure.

Dar es Salaam. Baadhi ya wananchi wanaotumia king’amuzi cha Star Times wamelalakimikia kutoonekana kwa chaneli tano za televisheni za ndani ya nchi kwa zaidi ya miezi miwili, licha ya kutakiwa kuzionyesha bure.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema awali, walikuwa wakizipata chaneli za ITV, EATV, Star TV, Channel 10 na TBC1 bila malipo, lakini sasa wanapata TV1 na TBC1 pekee.
Mkazi wa Mwenge jijini hapa, Razack Kazembe alisema awali alikuwa anapata chaneli hizo, lakini kwa sasa hazipati na alipouliza kituo cha huduma kwa wateja cha Star Time aliambiwa anatakiwa kulipia.
Kanuni ya 7(a) ya Kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta ya mwaka 2011 inazitaka kampuni zenye leseni ya miundombinu ya dijitalali (multiplex operator) kurusha chaneli tano za ndani bure na inayokiuka inatakiwa kulipa faini isiyopungua Sh5 milioni.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Star Media, Gasper Ngowi alisema hawajaanzisha utaratibu wa kutoza malipo chaneli hizo za bure na kuwataka wananchi wasioziona kufika ofisini kwao.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Innocent Mungy alisema wanatambua kuwa StarTimes inatoa huduma bure kwa chaneli tano za Kitanzania na kwamba uchunguzi ukibaini taratibu zimekiukwa sheria itafuata mkondo wake.

Source Mwananchi:->http://www.mwananchi.co.tz
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment