Image
Image

Watu watano waarifiwa kuuawa baada ya bomu kulipuka Mogadishu.


Bomu kubwa limelipuka nje ya hoteli moja katikati ya Mogadishu karibu na lango la jumba la rais nchini humo.
Takriban watu watano wameripotiwa kuuawa.Kundi la wapiganaji wa Alshabab limekiri kutekeleza shambulio hilo.
Mtu mmoja aliyeshuhudia mlipuko huo amesema kuwa ameona watu wengi wakiwa wamejeruhiwa.Amesema kuwa hoteli hiyo imeharibika vibaya na kwamba vikosi vya usalama vimewasili katika eneo hilo.
Vyombo vya habari vinasema kuwa mkutano wa usalama ulitarajiwa kufanyika katika hoteli hiyo ya SYL.
Hoteli hiyo imeshambuliwa mara kadhaa na al-Shabab katika miaka ya hivi karibuni.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment