Image
Image

Waziri Nchemba ataka Majambazi waliotekeleza Mauaji ya Askari 4 kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

                      Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, MWIGULU NCHEMBA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, MWIGULU NCHEMBA amelaani vikali mauaji ya Askari wa nne yaliyotekelezwa na Majambazi 14 wakati polisi wakibadilishana lindo katika Benki ya CRDB  Tawi la Mbande Temeke jijini Dar es Salaam nakutaka wahusika wakamatwe mara moja nakufikishwa kwenye mkono wa sheria.
Waziri Nchemba ambaye ameonekana kuwa na huzuni kubwa na uchungu kufuatia mauaji hayo amefika katika eneo hilo la tukio na pia kwenda kuwajulia hali majeruhi ambao ni askari huku akijionea hali ilivyokuwa ambapo ameagiza kufanyika kila linalowezekana wauaji hao wapatikane mara moja.
Kwaupande wake Askari aliyenusurika kuuawa katika tukio hilo amesema kuwa Majambazi hao walipofanya tukio hilo la mauaji walikuja wakiwa na pikipiki tano ambapo walipakizana kila pikipiki watu wawili ambapo kila mmoja alikuwa na bunduki yake ambapo mara baada ya kushuka katika pikipiki walianza kuelekezea silaha zao eneo la benki kabla ya kuwaua askari hao wa nne.
Amesema kuwa baada ya kuelekeza Bunduki eneo la Benki walijipanga imara ambapo wengine walielekeza bunduki zao kuwashambulia na ndipo wakatekeleza mauaji hayo ambapo kwake yeye askari huyo alipigwa risasi ya mguuni ikatokea upande mwingine.
Kufahamu zaidi Play Video hii kuona na kusikia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment