Image
Image

Serikali kupitia upya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji (RUBADA).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itapitia upya sababu za kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) kufuatia mamlaka hiyo kuendeshwa kwa ubabaishaji.
Hatua hiyo imekuja baada ya mamlaka hiyo kushindwa kusimamia uendelezaji wa bonde hilo na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ikwiriri mkoani Pwani.
Alisema baada ya mapitio hayo shughuli za mamlaka hiyo zitahamishiwa kwenye mamlaka nyingine za serikali kwani RUBADA  imeshindwa kufanyakazi hiyo kwa muda mrefu.
“RUBADA wamepewa ardhi lakini wameshindwa kuiendeleza, tutafanya upya mapitio ya kuanzishwa kwake,” alisema.
Akizungumzia kuhusu Kampuni ya Agro Forestry Plantation inayotaka kujenga kiwanda cha sukari wiyani Rufiji aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha asilimia 60 ya watumishi watakaowaajiri wawe ni vijana wa wilaya hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, kwenda wilayani Rufiji kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Mkuranga na Ikwiriri.
Waziri Mkuu amelitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Ikwiriri kuhusu kutotatuliwa kwa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.
Naye Mkurugenzi wa halshauri ya wilaya hiyo, Rashidi Salum alimweleza Waziri Mkuu kuwa, mgogoro huo umeshatatuliwa kwa ngazi ya wilaya  hivyo hatua iliyosalia ni kwa uWaziri wa Ardhi kufika na ramani ili kutoa uamuzi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment