Image
Image

Wanawake 12,581 wafanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.

WANAWAKE 12,581 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mbeya katika kipindi cha kuanzia mwaka 2012 hadi Juni 2016. Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina, kati ya wanawake hao waliofanyiwa uchunguzi, 1,483 walibainika kuwa na dalili za awali za ugonjwa huo na kati yao 803 walipatiwa tiba mgando na wengine 246 walioonekana kuwa na dalili za saratani na walipewa rufaa kwenda Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Alibainisha hayo jana alipofungua mkutano wa siku tatu wa uraghibishaji kuhusu saratani ya shingo ya kizazi unaofanyika mkoani Mbeya unaohudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya ya uzazi mkoani humo ukiwa umeandaliwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA).
Alisema huduma zilizofanyika katika kipindi hicho zimetokana na ushiriki wa karibu wa wadau mbalimbali, likiwemo Shirika la Watu wa Marekani linalojishughulisha na Mapambano dhidi ya Ukimwi la Watereed lililofadhili katika kufundisha watumishi na kununua vifaa.
Alisema kutokana na ufadhili wa Watereed hadi sasa mkoani Mbeya vituo 18 vinatoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi na mwezi uliopita vituo 36 vimefundishwa na sasa watumishi wanasubiri kupewa vifaa mapema mwezi ujao ili waanze kutoa huduma.
Mratibu wa Mradi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kutoka Wama, Dk Sarah Maongezi alisema lengo ni kuhamasisha timu za afya za mikoa ya Mbeya, Mwanza, Iringa, Mbeya na Mara na wilaya zake na kuona mafanikio yaliyopatikana kutokana na mikakati iliyowekwa mwaka 2014.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment