Image
Image

Kambi ya wanajeshi wa Djibouti yashambuliwa Somalia.

Wanajeshi kadhaa waripotiwa kufariki katika shambulizi lililotekelezwa dhidi ya kambi ya jeshi la Djibouti katika mji wa Beledweyne nchini Somalia.Mtu mmoja aliekuwa katika gari lililokuwa na vilipuzi amejitoa muhanga karibu na mlango wa kambi ya wanajeshi ktoka Djibouti katika mjini wa Beledweyne nchini Somalia.
Shambulizi hilo limetokea Jumanne katika kitongoji cha Hiiraan.
Msimamizi  wa masuala ya kisiasa na usalama katika mkoa wa Hiiraan Mohamed Amin alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari .
Wanajeshi kutoka Djibouti waliwasili nchini Somalia chini ya ombi la AMISOM kushiriki katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment