Image
Image

Mikopo ya Elimu ya Juu; Rais Akiri hakukuwa na Usimamizi mzuri*aagiza mamlaka husika kumaliza tatizo hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli yuko Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiweka jiwe la msingi kwenye Majengo mapya kwa ajili ya Malazi ya Wanafunzi.
Akihutubia Chuoni hapo, Rais amezungumzia suala baadhi ya Wanafunzi kudaiwa kukosa Mikopo.
Rais amesema mwaka huu Serikali yake imeongeza fedha kwa ajili ya Mikopo ya Wanafunzi na watatoa Mikopo kwa Wanafunzi wengi kuliko mwaka uliopita.
Hata hivyo Rais alisema " Naomba nikiri kwamba hakukuwa na Coordination nzuri. Kwanza ilipaswa Vyuo vyote vifunguliwe siku moja ili kuwe na mawasiliano mazuri. Lakini kilichotokea sasa kuna vyuo vimefunguliwa wakati Wanafunzi hawajui watapata Mkopo au hawatapata. Na cha kusikitisha Vyuo vinakataa kuwafanyia 'Registration' . Jambo hilo sio jema linasababisha usumbufu kwa Wanafunzi".
Rais ameiagiza Wizara husika, Bodi ya Mikopo na Taasisi zote zinazohusika kumaliza haraka tatizo hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment